Jumamosi 28 Februari 2026 - 06:00
Kuandaliwa msafara mpya wa kimataifa kwa ajili ya azma ya Palestina

Hawza/ Waandaaji wa kampeni hii mpya wameutaja kuwa ni msafara mkubwa zaidi wa kuonesha mshikamano na Palestina, na wamesema kwamba safari hii mbali na njia ya baharini, njia ya ardhini pia imezingatiwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, inatarajiwa kwamba mkono wa baharini wa msafara huu mkubwa utajumuisha zaidi ya meli mia moja; vilevile miongozo ya kuupanua zaidi na kuvutia washiriki kutoka nchi mbalimbali inaendelea kufanyiwa uchambuzi.

Safari hii, miongoni mwa meli hizo kutakuwepo vituo vilivyoandaliwa kwa ajili ya huduma za dharura za afya, vikiwa na madaktari, wauguzi na kliniki zinazotembea. Aidha, vituo kwa ajili ya uwepo wa wataalamu wa kurekebisha miundombinu ya kiraia iliyoharibiwa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza vimetayarishwa.

Waratibu wa msafara huu wameeleza wazi lengo lao kuu kuwa ni kuondoa mzingiro ambao umegeuza maisha ya kila siku ya watu wa kawaida kuwa mtihani mgumu, na wote wamesisitiza kwamba uhai wa raia na watu wa kawaida haupaswi kamwe kuwa jambo la kujadiliana.

Wameongeza kuwa; Rafah kama mpaka ulipaswa kuwa njia ya kupita, lakini sasa umegeuzwa kuwa eneo lililofungwa bila kupitika, ambako majeruhi husubiri bila matumaini; familia zimetenganishwa na wanafunzi wamebaki wamekwama nyuma yake huku fursa zao zikiwa zimepotea.

Chanzo: SAFA NEWS

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha